Wednesday, July 4, 2012

TANZANIA FOOTBALL NEWS: NIYONZIMA ARUDI YANGA

Kiungo wa Kimataifa raia wa Rwanda,Haruna Niyonzima Fabregas amerejea juzi usiku na kujiunga na Kikosi cha Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati Young Africans Sport Club (YANGA) katika mazoezi yaliyoanza jana majira ya saa kumi katika uwanja wa Kaunda Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na tovuti ya klabu www.youngafricans.co.tz kiungo huyo amesema kuchelewa kwake kulitokana na matatizo binafsi yaliyokuwa yamemkuta wakati akiwa nchini kwao na kusababisha kuchelewa kujiunga na Kikosi chake.

Haruna amewataka wachezaji wenzake kurejesha heshima kwa mara nyingine kwa kutwaa kombe la Kagame katika michuano inayotarajiwa kuanza Julai 14 Mwaka huu, huku Yanga ikiwa ndiyo Mabingwa watetezi wa michuano hiyo.

Niyonzima amesema tangu alipokuwa mapunziko alikuwa akifuatilia kwa karibu juu ya Klabu yake ya Yanga hasa katika zoezi la usajiri unaoendelea na kupongeza usajili huo kutokana na baadhi ya wachezaji anaowafahamu kusajiriwa katika kikosi hicho.

Yanga itaanza kutupa karata yake dhidi ya Atletico ya Burundi ambapo mechi hiyo ndiyo itakayokuwa ni pekee wakati wa ufunguzi itachezwa katika uwanja wa Taifa,Jijini Dar es Salaam huku Simba ikaanza kampeni siku inayofuata.

TUJIKUMBUSHE: JAVIER MARTINEZ WA ATLECTICO MADRID ATIMULIWA KUPIGA PICHA SIKU HISPANIA ILIPOCHUKUA KOMBE LA EURO 2012

Wakati Spain walipokuwa wamekabidhiwa kombe lao la Euro wachezaji wa Barcelona na Real Madrid walianza kuchukua kombe na kuanza kupiga nalo picha kwa kila kundi la wachezaji wa timu hizo mbili kupiga picha ya pamoja na kombe.


Walianza Barceona ambao wao ndio wengi kwenye kikosi cha Spain wakapiga picha na kombe kisha wakawabidhi wa Real Madrid - wakiongozwa na nahodha Iker Casillas, Raul Albiol, Arbeloa, Xabi Alonso na Sergio Ramos walijipanga kupiga picha na kombe na ghafla akaibuka Javier Martinez wa Atletico Madrid na kujipanga nao - kwa utani mchezaji mwingine akisaidiana na Sergio Ramos wakamtoa kwenye sehemu ya kupiga picha hiyo maalum kwa wachezaji wanaochezea Madrid.

TANZANIA FOOTBALL NEWS: SIMBA YAIKUNG'UTA MAFUNZO 2-1

Siku moja baada ya kutoka sare na klabu ya Express ya Uganda, mabingwa wa Tanzania bara klabu ya Simba imeanza vyema michuano ya kombe la Urafiki huko Zanzibar baada ya kuwagonga wala urojo klabu ya Mafunzo   kwa mabao mawili kwa moja.

Alikuwa ni kinda jipya la klabu hiyo lilosajiliwa kutoka klabu ya Ruvu Shooting aliyefunga mabao ote mawili katika dakika ya 27 na 44, huku pasi za mwisho zote zikitolewa na kiungo mpya wa timu hiyo Kanu Mbivayanga raia wa DRC Congo.

Kwenye dakika ya 80 Mafunzo walikuja juu na kufanikiwa kufunga bao la kufutia machozi  lililofungwa Jaku Joma

Timu zilianza hivi
Simba; Juma Kaseja, Haruna Shamte, Amir Maftah/Paul Ngalema, Lino Masombo, Shomary Kapombe, Amri Kiemba, Danny Mrwanda/Mwinyi Kazimoto, Mussa Mudde/Paul Ngalema, Abdallah Juma/Uhuru Suleiman, Kanu Mbivayanga/Haroun Othman na Kiggi Makassy.

Mafunzo: Suleiman Janabi, Hajji Abdi, Ally Juma, Yussuf Makame, Said Mussa, Juma Othman, Abdulrahim Mohamed, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Ismail Khamis, Juma Jaku na Ally Othman.