Wakulima wa zao la kahawa wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya,wamesema biashara ya uuzaji wa kahawa Mbichi imekuwa ikiendelea kufanyika licha ya Serikali ya mkoa kupipiga marufuku biashara hiyo kutokana na baadhi ya watendaji wa Serikali kujihusisha na ununuzi wa kahawa hiyo.
Wakiongea na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti wa kulima wa zao hilo katika kata ya Mlangali wilayani humo wamesema mtandao wa biashara ya kahawa mbichi (CHERRY) umekuwa ukifanywa na watendaji wa Serikali kupitia mawakala ndiyo maana wameshindwa kuwadhibiti. Aidha mmoja wa wakulima hao Batholomeo Mwayela wamesema mkulima anayeuza kahawa mbichi hupata hasara zaidi ya mara tatu ukilinganisha na bei ya kahawa inayokobolewa.
Kwa upande wake Afisa kilimo wa kijiji cha Lukululu kata ya Mlangali Bi.Miriam Philipo amewataka wakulima kuwa na tabia ya kuweka akiba ya fedha ili ziweze kuwasaidia katika msimu wa mavuno.
Wakati huohuo amesema wakulima wamekuwa wakipata hasara kubwa kupitia biashara hiyo na Serikali imeombwa kusimamia soko la zao la kahawa ili kuwezesha kuwepo kwa bei itakayomnufaisha mkulima kutokana na kutokuwepo kwa bei maalumu katika msimu wa mavuno wa zao hilo.
No comments:
Post a Comment