Tuesday, July 3, 2012

AFRICA NEWS: MUGABE AKIMBIZWA SINGAPORE KWA MATIBABU

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amepelekwa tena nchini Singapore kwa ajili ya matibabu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe ametangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, lengo la Rais Mugabe la kuelekea tena nchini Singapore ni kuangalia afya yake.
Mugabe mwenye umri wa miaka 88 amekuwa Rais wa Zimbabwe tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake Aprili 18, 1980 kutoka kwa mkoloni mkongwe wa Ulaya, Uingereza.
Imetangazwa kuwa, Rais Mugabe atarejea nchini humo mwishoni mwa wiki ijayo baada ya kufanyiwa matibabu nchini Singapore.
Inadaiwa pia kuwa Rais huyo wa Zimbabwe anasumbuliwa na maradhi ya kensa

No comments:

Post a Comment