Jumla ya Nyumba 150 na ghorofa 5 zitajengwa na Shirika la Nyumba nchini katika mkoa wa Mbeya katika maeneo ya Lupaway na Forest .
Akizungumza na waandishi habari Meneja wa Shirika la Nyumba mkoani Mbeya Bwana Malisa amesema maandalizi ya mradi huo yamekamilika mpaka sasa ambapo nyumba 150 zitakuwa za makazi na ghorofa 5 zitakuwa za biashara.
Kuhusu nyumba za biashara Bwana Malisa amesema kitalu namba 2/4 kilichopo Lupaway Jijini Mbeya kitahusika katika mradi huo.
Hata hivyo amesema Shirika la Nyumba nchini limemilikishwa eneo lenye ukubwa wa ekari 26 Iwambi jijini hapa na kuongeza kwamba hatua za kuliandaa kwa jili ya ujenzi zimeshaanza.
Aidha amesema Shirika hilo lipo kwenye mchakato wa kupata ardhi katika eneo la Songwe Viwandani, Ikumbi na Mwashiwawala kwa ajili ya ujenzi wa Mji wa Satelite na kuwa na matokeo mazuri baada ya kukamilika ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe.
No comments:
Post a Comment