Thursday, June 28, 2012

TANZANIA ENTERTAINMENT NEWS: SHIWATA YASOGEZA MBELE TAMASHA HADI AGOSTI 21/22


M
TANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umesogeza mbele tamasha la Watani wa Jadi  lililokuwa lifanyike 1/7/2012 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hadi Sikukuu ya Iddi Mosi ambayo inatarajiwa kuwa 21 au 22 Agosti mwaka huu.
Tamasha hilo ambalo linawakutanisha Timu ya Simba Veteran na Yanga Veteran pia kutakuwa mchezo wa mieleka kati ya msanii wa filamu, Lumole Matovolwa (Big) na Roman Mng’ande (Romario) wa Msondo wanawake watakaopambana katika mieleka ni Mwajuma Jimama na Sophia Lubuva kutakuwa na Ngongoti Basketball.
 
Vikundi maarufu vya ushangiliaji Mpira Pesa  cha Simba na Yanga Bomba (Yanga) vitapambana katika mchezo wa soka na baadaye kushangilia timu zao zikimenyana na bendi ya Msondo Music Band itatumbuiza.
 
Limeosogezwa mbele ili kutoa nafasi ya kutosha kwa ajili ya maandalizi ya timu za Simba na Yanga Veteran ambazo zitapambana siku hiyo, pia kutoa nafasi kwa mashabiki na watoto wengi zaidi kuweza kuhudhuria.
 
Pia filamu iliyochezwa na SHIWATA ya Kisufuria itazinduliwa. iliyowashirikisha wasanii maarufu kama Ahmed Olotu (Mzee Chilo), Big, Nisha, Haji Mboto na Mama Mau.
 
Madhumuni ya Tamasha hilo ni kukusanya fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba za Wasanii na Waandishi wa Habari, zinazojengwa katika Kijiji cha Mwanzega, Mkuranga ambazo mpaka sasa nyumba tano (5) za kisasa zimejengwa.
 
Mwenyekiti wa SHIWATA,Cassim Taalib alisema  kiongozi wa Yanga Veteran Bakari Malima (Jembe Ulaya) na kiongozi wa Simba Thomas Kipese wametamba kuonesha kazi siku hiyo.
 
Kipese akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema kuahirishwa kwa mpambano wao kunawapa nafasi wachezaji wake kujiandaa vizuri kwa mazoezi, naye Malima alisema wachezaji wake wako fiti wakati wote watakapohitajika kuingia uwanjani watashinda pambano hilo.
 
Wachezaji wa Simba wanajiandaa na pambano hilo ni Madaraka Suleiman, Abdul Mashine, Barnabas Sekelo, Said Kokoo, Boniface Pawasa,
Duwa Said, Mrisho Moshi,  Kamba Lufo, Malota Soma, Shabani Kisiga, Abubakar Kombo, Iddi seleman, Majuto Komu, Ramdhani Waso, Kelvin Mhagama, Issa Manofu na Kipese.
 
Nao wachezaji wa Yanga wanajiandaa na pambano hilo ni Peter Manyika, Mzee Abdallah, Anwar Awadh, Kenny Mkapa, Salvatory Edward, Shabani Ramadhani, Abdul Maneno, Steven Nyenge, Mohamed Hussen (Mmachinga), Edibilly Lwinyamila, Sekilojo Chambua, Thabit Bushako, Ally Mayay, Banza Tshikala na Malima.
 
 
Msemaji wa SHIWATA, Peter Mwenda
 
0786/0752/0715 222677
0776 222115

No comments:

Post a Comment