Thursday, June 28, 2012

MBEYA UPDATE: WATU 3 WAFA


M
toto mchanga ambaye hajafahamika kwa jina na anuani amekutwa amefariki dunia baada ya kutupwa kandokando ya mto Sinde, jana saa 4 asubuhi jijini Mbeya.

Taarifa kutoka kwa kamanda wa polisi na kamishna msaidizi mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani zimeeleza kuwa mtoto huyo mwenye jinsi ya kiume amekutwa ametupwa  na mtu asiyejulikana chini ya daraja, kandokando ya mto Sinde, jijini Mbeya.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya na jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.

Aidha kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani ametoa wito kwa mwananchi yeyote mwenye taarifa juu ya tulio hili ajulishe kituo cha polisi chochote kilichopo jirani naye ili hatua za kisheria zichukuliwe

Watu 2 wamefariki dunia na wengine 15 wamejeruhiwa huku 3 kati yao wakiwa na hali mbaya katika ajali ya gari iliyo tokea jana saa 11:30 jioni katika kijiji cha Chiwanda, wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya katika barabara ya Tunduma –Mbeya.

Habari kutoka polisi zinasema ajali hiyo imetokea katika eneo la kijiji cha Chiwanda wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya wakati gari mali ya Fanta Shiru yenye namba za usajili T 289 ACB/T 133 CAN, aina ya Scania Pulling lililokuwa limebeba soda mali ya kampuni ya pepsi iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aliye fahamika kwa jina moja la Masoud likitoka Mbeya kuelekea Sumbawanga.

No comments:

Post a Comment